October 31, 2020

VIFAA KUENDELEZWA KUSHUSHWA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said, ambaye alisafiri kwenda jijini Kinshasa, DR Congo kumaliza biashara kuwanyakua Tuisila Kisinda na Tunombe Mukoko, ameliambia chanzo chetu kuwa kazi ya kukisuka upya kikosi cha Yanga inaendelea kwa weledi mkubwa na siku si nyingi watamaliza kila kitu.

Hersi alisema wanataka kuona Yanga inakuwa imara kila idara na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na mashindano mengine inakuwa na kikosi cha kushindania mataji.

“Tuko imara na hatuyumbi kabisa, tunaendelea kuimarisha timu kila idara na majibu yatapatikana uwanjani. WanaYanga wasihofu kabisa, kila kitu kinakwenda vizuri,” alisema Hersi ambaye leo atatua nchini akiwa ameongozana na mastaa hao wapya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *