October 28, 2020

JEZI MPYA YANGA KUZINDULIWA DODOMA

Msomaji wa Yanganews Blog:Klabu ya Yanga SC, imetangaza rasmi kuwa uzinduzi wa SportPesa wiki ya Mwananchi utafanyika Jumamosi ya Agosti 22 mjini Dodoma kwa kufanya matembezi ya hiari na wanachama wa klabu hiyo.

Matembezi hayo, yameelezwa yataanzia makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Dodoma karibu na Uwanja wa Jamhuri huku wakipita Dodoma Inn (Bungeni) kueleleka Viwanja vya Mashujaa ambapo kutakua na michezo, uchangiaji damu na burudani kadha wa kadha.

Akizungumzia uzinduzi wa huo na kutoa ratiba kamili ya namna ambavyo wiki hiyo itaendeshwa,  Mwenyekiti wa Habari na Hamasa, Suma Mwaitenda amesema, ”Jumamosi tutaanza na matembezi lakini pia tutakuwa na vikao vya matawi na vikundi vya washabiki nchi nzima kwenye maeneo yao kupanga mikakati ya ushiriki wao”

“Siku itakayofuata tutatoa huduma katika maeneo na makundi stahiki, ikiwemo yatima na wazee lakini pia tutafanya usafi na upandaji wa miti ili kutunza mazingira yetu,” amesema Mwaitenda

Mwaitenda ameeleza kuwa Agosti 28 ndio siku ambayo wataitumia kufanya utambulisho wa jezi ambazo watazitumia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, “Lakini pia mashabiki na wadau wa Yanga tutaitumia siku hiyo kuchangia damu kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam ambako kilele cha wiki yetu kitakuwa Agosti 30,” amesema.

Upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji SportPesa nchini, Abbas Tarimba alitumia fursa hiyo kuipongeza Yanga kwa kitu kikubwa ambacho wanaenda kufanya mbele yao huku akitoa ahadi kuwa wataendelea kushirikiana nao bega kwa bega.

“Tutajitahidi kuendelea  kushirikiana  nao na hata katika uzinduzi wa  Sportpesa  wiki ya Mwananchi  nadhani tutakuwepo lakini nitumia fursa hii kuwapongeza kwa tukio kubwa ambalo lipo mbele yao, hakuna soka Tanzania bila ya uwepo wa Simba na Yanga,” amesema.

Yanga leo Agosti 20 wamewapokea majembe yao mawili kutoka Congo amano ni Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wataungana na wenzao walioanza mazoezi kujianda na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi kuwapokea na jambo ambalo liliibua furaha kwa mashabiki ni pale walipotengeza kiti na kumbeba juu Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga, Hersi Said

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *