October 28, 2020

JIJI LIMETIKISIKA ‘MAPOKEZI TUISILA, TONOMBE YANGA’

Msomaji wa Yanganews Blog:Nyota wapya Yanga, Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko leo, Agosti 20 wamewasili rasmi ndani ya ardhi ya Tanzania.

Mapokezi ya nyota hao yameweka rekodi kwa mashabiki wengi wa Klabu ya Yanga kujitokeza kuwapokea.

Safari ilianzia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo huko shangwe lilikuwa la kutosha.

Kisha shangwe likatua mpaka makao makuu ya Yanga, mitaa ya Jangwani.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said alibebwa juu mithili ya mfalme kwa kuwa alihusika kwenye kukamilisha dili hilo.

Nyota hao wote wawili wamesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga ambayo inaendelea kuboresha kikosi chake baada ya kuwaacha nyota wake 16.

Pia wote walikuwa wanakipiga ndani ya Klabu ya AS Vita ya Congo moja ya klabu kubwa nchini Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *