October 28, 2020

ALICHOSEMA MKURUGENZI GSM BAADA UJIO SARPONG YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Straika mpya wa Yanga, Michael Sarpong amejikuta kutoamini kile alichokutana nacho baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3.

Sarpong baada ya kutoka mlango wa wageni wanaowasili akipokelewa na Injinia Hersi Said, alikuta mashabiki wa Yanga wakipiga makofi muda wote huku wakiimba jina lake pamoja na kutaja GSM ambao ni wadhamini wao.

Mchezaji huyo alijikuta akionyesha sura ya tabasamu tu muda wote na kusema “Nashukuru kwa mapokezi mazuri mliyonipatia, nashukuru sana”.

Baada ya kuzungumza hayo, Hersi naye amesema “Huu ni mwendelezo wa kukijenga kikosi chetu kwaajili ya kuwa na timu nzuri msimu ujao, bado wachezaji wawili mmoja eneo la kiungo na mwingine mshambuliaji na wote watatua huku upande wa kocha yeye ni Jumatatu na tutatoa taarifa”.

Baada ya kutoka nje na kutembea kwenda kwenye gari la Hersi aina ya Mercedez Benz G63, mashabiki walilizunguka gari hilo na kuanza kuimba kwa shangwe.

Walipoona hilo halitoshi waliamua kufuta barabara kwa mikono ili gari hiyo ipite huku wengine wakiwa wanalifuta kama vile wanaliosha.

Tukio hilo liligeuka kuwa kivutio hata kwa wao wenyewe kwani walionekana kulifanya huku wakiwa na nyuso za furaha.

Baada ya kufanya mambo yao yote hayo kwaajili ya kumpokea mchezaji huyo, waliamua kufanya dua kwa pamoja.

Jambo hilo lilipokelewa vizuri na Sarpong, Hersi pamoja na Msomali Kibonge ambao walikuja kumpokea mchezaji huyo.

Walipomaliza kusali Hersi aliwasha gari kisha kuondoka huku mashabiki wakilifata nyuma hilo gari wakiwa wanaimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *