October 28, 2020

MSOLLA KULIANZISHA WIKI YA MWANANCHI DODOMA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla leo atawaongoza wanachama, wapenzi na mashabiki wa Timu ya Wananchi, katika tukio la uzinduzi wa tamasha la Sportpesa Wiki ya Mwananchi jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Uzinduzi, Albinus Dominick amesema, Dkt. Msolla pamoja na kushiriki uzinduzi pia atawaongoza wanaYanga katika matukio mengine ikiwamo mazungumzo ya kimkakati kuelekea kwenye ujenzi wa sura mpya ya klabu ambayo yatafanyika jioni ikiwa ni sehemu ya shughuli za tukio la uzinduzi.

“Mwenyekiti wetu ndio atakuwa mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi, wadhamini wetu wote watashiriki pia, hivyo kwa siku ya leo Dodoma itatawaliwa na Kijani na Njano, rangi zetu Wananchi,” amesema.

Amesema kuanzia asubuhi WanaYanga wanakutana tawi la Yanga Makao Makuu, Kisha kufanya matembezi ya mshikamano kuelekea viwanja wa Mashujaa ambapo shughuli nzima ya uzinduzi itafanyika na baadaye kutakuwa na mechi kati ya Tawi ya Dodoma na Wanachama kutoka maeneo mengine mechi itakayochezwa Uwanja wa shule ya sekondari Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *