October 25, 2020

ALICHOSEMA MSOLLA BAADA YA UJIO WA SENZO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kitendo cha kumuongeza raia huyo wa Afrika Kusini, ni kuongeza nguvu katika harakati za mabadiliko.

“Baada ya kuingia mkataba na La Liga tulimuomba mdhamini wetu Kampuni ya GSM ambaye anasimamia mabadiliko kuongeza wataalamu katika harakati hizo ndipo walianza kutafuta mtu na hatimaye tukampata Senzo, ambaye tunaamini atatusaidia kufika tunapopataka,” amesema Dkt. Msolla katika Uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi jijini Dodoma.

Dkt. Msolla amesema Senzo anakuja kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha Utendaji wa kisasa kwenye klabu hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko na kwanza atajenga mwanzo mzuri kuelekea kwenye Dira ya maendeleo ya klabu.

“Kama mnavyofahamu hivi sasa tupo katika kipindi cha awali cha miezi mitano ya mwanzo ya mabadiliko hivyo tunahitaji watu wenye utaalam katika kila eneo ili tusonge mbele,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *