October 28, 2020

WACHEZAJI WAZAMANI YANGA KUONGEZA HAMASA KILA TIMU INAPOKWENDA

Msomaji wa Yanganews Blog:kuongeza morali na hamasa ya wachezaji wanaoicheza Yanga, wachezaji waliowahi kung’ara na timu miaka ya nyuma, watahusika kwenye kila mchezo wa timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza Septemba 6 mwaka huu.

Wachezaji hao ambao kwa kiasi kikubwa walishiriki kuipatia mafanikio timu hiyo, watatambuliwa rasmi na uongozi wa timu hiyo ambapo watasafiri na timu hiyo popote itakapokwenda kucheza mchezo wa mashindano yote.

Akizungumzia hilo hilo leo Jumapili Agosti 22, 2020 wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi, Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla amesema katika wachezaji hao waliowahi kuichezea timu hiyo miaka ya nyuma, watagawana kila mchezo atahusika mchezaji mmoja tu na wengine watasubiri mchezo utakaofuata kwa mtiririko maalum.

“Katika kuhakikisha kwamba wachezaji wanaoitumikia timu yetu hivi sasa wanakuwa na ari na uchungu kwa timu, tumeamua kuwashirikisha wachezaji wetu wa zamani kusafiri na timu popote tutakapocheza mechi zetu” amesema Dk Msolla.

Akitolea mfano wa nyota wa zamani wa timu hiyo, Edibily Lunyamila aliyekuwepo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi, Dk Msolla ameongeza kuwa, wachezaji hao watakuwa kambini na timu kwa maandalizi yote kabla ya kusafiri na timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *