October 28, 2020

JEZI MPYA YANGA KUZINDULIWA AGOSTI28

Msomaji wa Yanganews Blog:Wiki ya Mwananchi imezinduliwa rasmi jana jijini Dodoma katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo katikati ya jiji la Dodoma.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Mshindo Msolla ambapo pamoja na mambo mengine, ilitarajiwa kuzinduliwa jezi mpya za timu hiyo kwa msimu ujao wa ligi na mashindano mengine.

Hata hivyo, Dk Msolla alisema kutokana na kuendelea na zoezi la usajili wa wachezaji linaloendelea, uzinduzi wa jezi mpya utafanyika siku mbili kabla ya kuhitimisha wiki yao jijini Dar es Salaam, Agosti 30.

“Tunaendelea kukamilisha zoezi la usajili wa wachezaji wetu ikiwemo wawili kutoka nje ya nchi”

“Kuhusu uzinduzi wa jezi utafanyika Agosti 28, 2020 jijini Dar es Salaam kabla ya kucheza mchezo maalum wa kirafiki siku mbili mbele” alisema Dk. Msolla.

Dk Msolla pia alimaliza kwa kukata utepe wa uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa wanachama wa Yanga mkoani Dodoma, Dominick Albinus.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *