October 28, 2020

SENZO ATINGA MAZOEZINI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Senzo Mbata jana Agosti 22 ameibuka ndani ya Uwanja wa Chuo cha Sheria kuwaona wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya wiki ya Wananchi pamoja na Ligi Kuu Bara.

Yanga ilianza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2020/21 Agosti 10 na mchezo wa kwanza kwenye ligi unatarajiwa kuwa Septemba 6 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.

Baada ya kufika mazoezini leo kwa mara ya kwanza, Mbatha alikutana na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa msimu huu kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko pamoja na Michael Sarpong.

Nyota wote wapya wa Yanga wanatarajiwa kutangazwa Agosti 30 kwenye kilele cha siku ya Wananchi ambapo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *