October 28, 2020

WANACHAMA YANGA ILALA WATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALINI ‘WIKI YA MWANANCHI’

Mwenyekiti wa Tawi la Chakenge, kata ya Msongola wilaya ya Ilala, ndugu Amrani amesema wameamua kutoa huduma kwenye hospitali ili kuonesha kuwa Yanga ni Timu ya Wananchi hivyo leo tukizindua Wiki ya Mwananchi wameamua kujumuika pamoja na kuweza kufanya usafi katika hospitali Wilaya ya Ilala, Kivule.

“Ujumbe wetu kwa wanaYanga wa Matawi mengine ni kuwa kujitolea ni mojawapo ya ishara ya kuimarisha upendo tujue kuwa sio tu kufanya usafi ndio njia bora katika Klabu yetu bali hata kutembelea wagonjwa au watoto yatima ni ishara ya kuonesha upendo kwenye jamii, ikumbukwe Dar Young Africans ni Timu ya Wananchi”

Mwenyekiti Amrani amegusia pia furaha waliyonayo kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara akisema, “Matarajio yetu ni ushindi tu. Tunashauri wachezaji wetu wawe wamoja, waoneshe nidhamu pia tunapenda kuupongeza uongozi wa Klabu yetu, wadhamini wetu SportPesa, GSM, Taifa Gas na wengine, kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye usajili na kuleta mabadiliko chanya kwenye timu yetu”.

WanaYanga wengine wanakaribishwa kutuma taarifa, picha na ‘videos’ za matukio wakiadhimisha Wiki Ya Mwananchi kwa kutuma ujumbe kwa WhatsApp kwenda namba 0677 045 863

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *