October 31, 2020

MSOLLA AWEKA MSISITIZO, MORRISON NI MCHEZAJI WA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla muda mfupi baada ya kuzindua rasmi wiki ya Mwananchi hapa Dodoma leo Jumamosi.

Dk Msolla ameliambia chanzo chetu kuwa bado wanamtambua Morrison ni mchezaji wao halali kwa misimu miwili ijayo, baada ya kumsajili Julai 14 kufuatia mkataba wa awali kumaliza.

Dk Msolla alisisitiza kuwa, mkataba wao waliomsainisha Julai 14 mwaka huu ni halali baada ya ule wa miezi sita waliomsainisha Machi 20 kumalizika.

“Morrison bado tunamtambua ni mchezaji wa timu yetu kutokana na kusaini naye mkataba Julai 14 kufuatia ule wa awali wa miezi sita tuliomsainisha Machi 20 kumalizika, bado ni mali yetu, hao Simba tunawaomba waje mezani wamnunue” alisema Dk. Msolla.

Kuonyesha kwamba hawabahatishi, Mwenyekiti huyo alifichua kuwa Jumatatu ijayo ndio siku rasmi watakayopeleka mashtaka yao kwa shirikisho la soka duniani (Fifa).

“Tuna madai yetu ya msingi na ambayo ni haki yetu, keshokutwa Jumatatu ndio tunapeleka mashtaka yetu rasmi kwa fifa ambao wataamua na kutupatia haki yetu ya msingi” alisisitiza Msolla.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *