October 28, 2020

NAAM….HUYU HAPA KOCHA MPYA YANGA

Msonaji wa Yanganews Blog:Leo Agosti 22, 2020 mabosi wa Yanga wamemtangaza rasmi kocha mkuu mpya.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msola ndiye aliyemtangaza rasmi Kocha Mrundi, Cedric Kaze kuionoa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Msolla, ambaye ndiye mgeni rasmi wa uzinduzi wa wiki ya Mwananchi hapa inayofanyikia jijini Dodoma mwaka huu, alisema Kaze atainoa timu hiyo kufikia mafanikio wanayoyahitaji.

“Mnaouliza kuhusu Kocha, tumeshampata Cedric Kaze kutoka nchini Burundi ambaye alikuwa Canada na taratibu zinaendelea za ujio wake nchini tayari kuanza kazi ya kuinoa timu yetu” alisema Msolla.

Mbali na hilo, Msolla pia alisisitiza kuwa Kocha huyo atakuwa na wasaidizi wake aliowapendekeza mwenyewe ikiwemo Kocha wa makipa tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *