December 6, 2020

KAZE AFANYA MABADILIKO KIKOSI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Mkuu wa Yanga amefanya mabadiliko matatu katika kikosi chake wakiwafuata KMC akipangua safu ya ushambuliaji yake.

Kwenye kikosi ambacho Kaze amepanga kuanza nacho amewaanzisha mshambuliaji Michael Sarpong ambaye katika mchezo uliopita wa nyumbani aliingia kipindi cha pili akitokea benchi lakini pia amemuanzisha kwa mara ya kwanza mshambuliaji mwingine mzawa Waziri Junior.

Mchezo uliopita kocha huyo alimuanzisha Yacouba Sogne ambaye leo ataanzia benchiĀ  akibadilishana na Sarpong.

Kiungo Deuse Kaseke naye amepata nafasi ya kwanza ya kuanza katika utawala wa Kaze akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima ambaye leo ataanzia benchi.

Kiungo mwenye mabao mengi katika kikosi hicho Mukoko Tonombe mwenye mabao mawili ameendelea kupata nafasi sambamba na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Hata hivyo Kaze hajaigusa kwa lolote safu yake ya ulinzi akiendelea kuwaamini kipa Metacha Mnata, beki wa kulia Kibwana Shomari, beki wa kushoto Yassin Mustapha na mabeki wa kati nahodha Lamine Moro na msaidizi wake Bakari Mwamnyeto.

Safu hiyo ya ulinzi imeonyesha umakini mkubwa ambapo mpaka sasa imefikisha dakika 450 sawa na mechi tano bila kuruhusu bao.

Mwenye benchi Kaze amewapa nafasi Kipa Farouk Shikhalo,beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’,kiungo Zawadi Mauya,Niyonzima,Farid Mussa ambaye alikuwa nyota wa mchezo katika timu hiyo akichaguliwa na mashabiki wa timu hiyo akianzia benchi, Yacouba na Ditram Nchimbi.

HALI ILIVYO UWANJANI

Yanga imekuwa ya kwanza kutinga uwanjani saa 8:17 mchana, huku kukitanguliwa na gari la usalama na kupokelewa na makomando wao getini.

Wakati timu hiyo ikiingia uwanjani, mashabiki waliokuwa katika mlango kuingia vyumbani, waliamsha shangwe wakati wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi wakishuka kwenye gari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *