December 6, 2020

MWALIMU KASHASHA:KAZE APEWE MUDA, YANGA ITAKUWA TISHIO

Msomaji wa Yanganews Blog:Juzi tumeiona Yanga ikicheza mechi yake ya kwanza ikiwa chini ya Kocha Mkuu mpya, Cedrick Kaze kutoka Burundi ambaye yeye timu hiyo imemchukua kuziba pengo la Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa hivi karibuni.

Nilichokiona ni mapema mno kuanza kumjadili kocha Kaze kwa kuangalia mchezo ule wa juzi ambao walicheza dhidi ya Polisi Tanzania na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwani anahitaji muda wa kuitengeneza zaidi timu, jambo ambalo haliwezi kutimia ndani ya muda mfupi. Hata hivyo yapo baadhi ya mambo ambayo yameonyesha taswira kuwa Kaze atayafanya ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa siku za usoni ambayo kupitia mchezo wa juzi dhidi ya Polisi, wengi watakuwa wameyang’amua.

Miongoni mwa mambo ambayo nimeyaona kwa Kaze ni kwamba anataka kuona timu inacheza mpira wa chini ili wachezaji wote waweze kushiriki kuuchezea mpira. Mkicheza mpira wa chini inakuwa ni rahisi kwa kundi kubwa la wachezaji kuuchezea tofauti na iwapo mnapocheza mpira wa juu ambao ni wachezaji wachache tu watakaonufaika kutokana na kutofautiana kwa maumbile. Hata hivyo ufanisi katika kufanyia kazi staili hiyo ya Kaze ulionekana kutokuwa juu na hilo bila shaka linachangiwa na ugeni wa wachezaji kwa staili hiyo ukizingatia kwamba kwa sasa wanabadilisha kutoka utamaduni waliouzoea kwenda katika utamaduni mpya.

Moja ya changamoto ambazo zilionekana kwa staili hiyo mpya ni wachezaji kupoteza mipira lakini pia unaweza kuona mchezaji kama Yassin Mustafa akishindwa kuover lap kama alivyozoea na hiyo ni kwa sababu hakukuwa na ule upigaji wa mipira mirefu.

Ili kuiona Yanga ikicheza soka safi na la kuvutia, inahitaji muda kwa sasa wapo katika transition ya kutoka kwenye matumizi ya high balls kwenda katika matumizi ya mipira ya chini. Ukicheza mipira ya juu unatakiwa kuwa na aerial skills na sasa wanaenda kuwa na matumizi ya grund skills. Akipewa muda nadhani ataweza kufanya vizuri zaidi siku za usoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *