December 6, 2020

KIKOSI KAMILI YANGA, KUPAA KESHO KUIFUATA KMC

 

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla ataongoza msafara wa wachezaji na viongozi itakapokwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili wa mchezo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Afisa Habari wa Timu ya Wananchi, Hassan Bumbuli amesema msafara wa Yanga kuelekea Kanda ya Ziwa utaondoka kesho alfajiri kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, ikiwa ni siku moja kabla ya kuivaa KMC FC.

“Msafara utakuwa na jumla ya watu 38, wakiwamo wachezaji 25 na utaongozwa na Mwenyekiti wetu, Dkt. Msolla,” amesema Bumbuli.

Amesema uamuzi wa kwenda na wachezaji wote umetokana na kutaka kumpa nafasi Kocha kuwa na vijana wake wote kuwafahamu zaidi kwani Timu itakuwa huko kwa siku nyingi.

“Tunakwenda na kikosi chote kwa sababu maalumu za kiufundi, tunampa nafasi Kocha kuendelea kuwa na vijana wake wote kwa kuwa tutakuwa Kanda ya Ziwa kwa siku zaidi ya 10,” amesema.

Ametaja wachezaji watakaokwenda kuwa ni pamoja na Metacha Mnata, Ramadhan Kabwili, Farouk Shikhalo, Paul Godfrey, Shomari Kibwana, Adeyum Saleh, Yassin Mustapha, Said Juma, Bakari Mwamnyeto, Lamine Moro na Abdallah Shaibu.

Wengine ni Mukoko Tonombe, Zawadi Mauya, Haruna Niyonzima, Feisal Salum, Carlos Carlinhos, Farid Mussa, Tuisila Kisinda, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Michael Sarpong
Juma Mahadhi na Waziri Junior na Abdullaziz Makame.

Viongozi wa benchi la Ufundi ni Kocha Mkuu Cedric Kaze, Juma Mwambusi, Vladimir Niyonkuru, Hafidh Saleh, Shecky Mngazija, Mahmoud Omary, Faried Cassiem na Elieneza N. Nsanganzelu

Viongozi wengine watakaokuwa safarini pamoja na Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Msafara, watakuwa ni QS. Suma Mwaitenda, Mahmoud Milandu, Amani Allan Kimweri na Tonias Otieno Jakanyango.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *