November 27, 2020

MAMA MANJI APIGWA RUNGU YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kamati ya Sheria na Nidhamu ya Klabu ya Yanga, imemsimamisha uanachama, Bi. Bahati Mwakalinga maarufu kama Mama Manji kujihusisha na shughuli zozote za Klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia leo tarehe 23/10/2020.

Uamuzi huo umetangazwa na Katibu wa Kamati hiyo Mh. Benjamin Mwakasonde, kwa mujibu wa Ibara 42.1 (f) ya Katiba ya Klabu ya Yanga ya mwaka 2010, ambayo imeipa mamlaka Kamati ya Sheria na Nidhamu kumsimamisha Uanachama Mwanachama yoyote wa Klabu ya Yanga.

Bi. Bahati Mwakalinga maarufu kama Mama Manji, amekutwa na hatia katika shitaka la kutoa maneno ya uongo, yasiyo na staha, ya kuudhi na ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, mwishoni mwa mwezi Juni na mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *