November 27, 2020

MECHI WATANI WA JADI KUPIGWA DIMBA LA UHURU AU KUAHIRISHWA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba, hati hati kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya matengenezo.

Mchezo huo uliopangwa kuchezwa tarehe  7 Novemba.

Taarifa kutoka ndani ya Bodi ya Ligi nchini imeleza kuwa michezo yote iliyopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21 yote imehamishiwa kwenye Uwanja wa Uhuru mpaka pale Uwanja huo utakapofunguliwa.

Uwanja huo ambao unatumika kwa klabu za Simba na Yanga kwenye michezo yao ya nyumbani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na hata ya kimataifa sasa italazimika kuhamisha michezo yao ya kimashindano kwenye Uwanja Uhuru ambao unachukua idadi ndogo ya mashabiki.

Aidha bodi ya Ligi imeelezea kuwa michezo yote ya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza iliyopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma imehamishiwa kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa kwa michezo ya Ligi Kuu na Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mechi za ligi daraja la kwanza mpaka hapo Uwanja utakapokuwa tayari kwa matumizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *