December 6, 2020

ALICHOSEMA MKURUGENZI GSM BAADA YA USHINDI MECHI DHIDI POLISI TANZANIA

Msomaji wa Yanganews Blog:Baada ya Yanga kuisambaratisha Polisi Tanzania bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa timu hiyo mhandisi Hersi Said, ameeleza mipango yao kama timu baada ya mchezo huo na kuahidi makubwa kwenye michezo ijayo.

“Tunafurahi kupata pointi tatu muhimu, huu ni mwanzo mzuri kwa kocha wetu mpya, Cédric Kaze na tunaamini huko mbele tunakoelekea ataweza kufanya makubwa zaidi ya haya.” amesema.

“Baada ya hapa tutasafiri kwenda Mwanza kwa ndege kwaajili ya michezo mitatu dhidi ya KMC, Biashara na Gwambina na tunatarajia kurudi Dar es Salaam na alama zote tisa tutakazovuna huko,” alisema Hersi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *