December 6, 2020

LEO PATACHIMBIKA DIMBA LA UHURU

Msomaji wa Yanganews Blog:Leo kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga itashuka dimbani kumenyana dhidi Polisi Tanzania, huo ukiwa mchezo wa ligi kuu utaopigwa dimba la Uhuru, saa 10 jioni.

Kuelekea mchezo huo, Kocha mkuu, Cedric Kaze, ametamba kufanya vizuri katika mchezo wa leo.

Ni mchezo wa kwanza kwa kocha Kaze tangu amejiunga na kikosi hicho hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaze alisema mchezo utakuwa mzuri sana na anaimani watashindani kwani tangu amekuja yupo na timu na anaona mwenendo ulivyo.

Alisema timu imefanya maandalizi ya kutosha na anaimani itaonyesha kiwango kizuri sana na wachezaji wanaifahamu Polisi Tanzania wengi wamewahi kucheza na timu hiyo wachache ndio hawaifahamu.

Viingilio katika mchezo huo, Mzungoko 5000/=, VIPB 10000/=, VIPA 15000/=.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *