November 27, 2020

YANGA KUKINUKISHA KESHO, MCHEZO WA LIGI KUU DHIDI POLISI TANZANIA

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho katika dimba la Uhuru, kuelekea mchezo wa kesho Oktoba 22, 2020 na kocha Cedric Kaze ametamka kwamba wako tayari kukutana na Polisi Tanzania.

Yanga inakutana na Polisi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho Uwanja wa Uhuru huku wakongwe hao wakiwa na kocha wao mpya Kaze.

Akizungumza leo Kaze amesema amemaliza kazi ya kuandaa kikosi chake ambapo anaona vijana wake wako tayari kwa mchezo huo.

Kaze amesema katika siku tano alizokaa na timu hiyo yapo ambayo waneyafanyia kazi katika kuwapa ubora wachezaji wake tayari kwa mchezo huo.

Kocha huyo ambaye atakuwa na dakika 90 za kwanza katika ajira yake ndani ya Yanga amesema kazi iliyobaki kwao kama makocha ni kuchagua wachezaji ambao wataongoza jahazi la kutafuta pointi tatu.

“Mashabiki wetu waje uwanjani kuwapa nguvu vijana wao,makocha tumemaliza kazi ya kuwapa njia ya ushindi wachezaji,”amesema Kaze.

“Tunawaheshimu Polisi lakini Yanga lazima icheze kwa kujiamini na kumiliki mpira ili tupate matokeo,imani yangu vijana watafanya vizuri ili kupata ushindi muhimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *