November 27, 2020

TUWEKANE SAWA WANAYANGA, HATMA YA RIEDOH, KOCHA WA VIUNGO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha wa viungo wa Yanga, Riedoh Berdien hayupo kwenye kikosi cha Yanga kwa muda usiopungua wiki mbili.

Berdien alibainisha kuwa wengi wanaamini yupo Afrika Kusini, lakini kwa sasa yupo katika majukumu ya kitaifa.

“Watu wengi wanafahamu nipo Afrika Kusini, nipo Gambia katika majukumu ya timu taifa (Bafana bafana), na wiki iliyopita tulicheza mechi ya kirafiki na Congo na kuwafunga bao 1-0.

“Baada ya kumaliza majukumu yangu nitawasikiliza kwanza viongozi wa Yanga ili kujua mwenendo wa mkataba wangu ambao unamalizika Januari kama utaendelea au kusitishwa.

“Siwezi kufanya uamuzi wowote kwa sasa, nafasi kubwa nawapa Yanga, ambao nipo na mkataba nao wa miezi mitatu kabla ya kumalizika na wao baada ya kutoa uamuzi ndiyo nitakueleza, hizi klabu muda wowote unaweza kusitishiwa mkataba.

Katika hatua nyingine Berdien alisema amepata ofa za kuhitajika na baadhi ya klabu, lakini si nyingi kama zilivyokuwa timu za taifa ambazo zinahitaji kumpa kazi ya moja kwa moja.

Msomaji wa Yanganews Blog:Ikiwa inasubiriwa hatma ya kocha huyo wa viungo, uongozi wa Yanga umeamua kumtafuta kocha wa viungo ambaye atahudumia timu kwa mda ambaye ni mtanzania, Elieneza Nsanganzelu ambaye alikuwa akifanya kazi hiyo pia katika kikosi cha Taifa Stars kwenye benchi la kocha Ettiene Ndayiragije.

Kocha huyo hajasaini mkataba wowote na Yanga bali ameombwa kwa muda mfupi kuwaimarisha wachezaji kikosini hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *