October 28, 2020

KAZE KUTUA LEO USIKU

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Cedric Kaze anayekuja kuinoa Yanga SC, yupo safarini kuja nchini Tanzania kwaajili ya kuanza rasmi majukumu yake mapya.

Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli, amethibitisha ujio wa Kocha huyo ambaye mapema leo alikuwa jijini Amsterdam Uholanzi, kwaajili ya kubadilisha ndege ya kumleta Tanzania.

Mtihani wa kwanza wa Kaze Yanga huenda utakuwa ni ule dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Oktoba 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kaze aliandika ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter jana, akielezea namna anavyojivunia kuwa Kocha wa mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

“Ninajivunia kuwa  kocha  wa timu yenye historia kubwa, mashabiki wa aina yake, moja ya timu bora Afrik. Pamoja tutafanya makubwa,”aliweka ujumbe huo akiwa ameambatanisha na picha ya tukio la wiki ya Mwananchi la mwaka huu, ambalo Yanga walijaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kaze anatarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nne usiku leo kwa ndege ya Shirika la Ndege la KLM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *