October 31, 2020

MKURUGENZI GSM AWEKEA UFAFANUZI USAJILI WA MSHAMBULIAJU BURUNDI

Msomaji wa Yanganews Blog:Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu mshambuliaji Said Ntibazonkiza baada ya kung’aa zaidi katika mchezo w Taifa Stars dhidi ya Burundi

Yanga imemsainisha mkataba wa miaka mwili mshambuliaji Said Ntibazonkiza baada ya kung’aa zaidi katika mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Burundi.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo atatua haraka nchini kuja kuanza kuitumikia klabu hiyo mara baada ya dirisha dogo kufunguliwa.

Hatua ya Yanga kuinasa saini ya mshambuliaji huyo imekuwa rahisi baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ikiwa ni hesabu za muda mrefu.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said amesema hesabu zao katika kumuwinda mshambuliaji huyo zilikuwa za muda mrefu lakini walishindwa kukamilisha awali katika dirisha lililopita kufuatia klabu yake kuweka ngumu kumuachia.

“Alikuwa na mkataba na klabu yake tukazungumza nao lakini hawakutaka kumuachia na muda haukuwa rafiki lakini sasa ameumaliza mkataba na yuko huru,” amesema Hersi.

“Amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza sasa na tumeshamalizana naye kila kitu nafikiri atajiunga na timu sio muda mrefu.

9 thoughts on “MKURUGENZI GSM AWEKEA UFAFANUZI USAJILI WA MSHAMBULIAJU BURUNDI

  1. Thіs paraagraph offers clear idea designed for ttһe new ⲣeople
    oof blogging, that genuinely how to do rrunning a ƅlog.

    Alsso vissit my blog; AWL settlement (Ellis)

  2. Jamani viongozi nimefuatilia sana timu yetu hakika kwanza sina budi kuupongeza uongozi wetu na watu wote wenye mapenzi na uchungu wa timu yetu hasa mfadhili na mwanachama wetu pendwa GSM kuhakikisha timu au chama la wananchi msimu huu tunapata tulichopanga kukipata kupitia maombi yetu kwa “Mungu Allah”. Basi nauomba uongozi wetu utulie na ujaribu kumpatia mwalimu mpya muda wa kutosha kuweza kuunganisha wachezaji na kujenga umoja na upendo baina ya wachezaji wanapokuwa uwanjani, pia nitoe maoni yangu kwa wachezaji watambue Yanga sio ya mchezaji mmoja uwanjani hivyo matokeo yoyote ni kwa ajili ya Yanga hivyo uchoyo au ubinafsi hautakubalika pale unapoona mwenzako yupo nafasi nzuri mpatie mpira afunge badala ya kulazimisha ufunge wakati unajua sehemu uliyopo kamwe huwezi na ndipo unapoiangusha timu na wananchi . Naamini msimu huu kuna jambo letu watuachie tulifanye hakika ipo siku watu watashangaa kitakachotokea uwanjani mtu atakapo weka mpira kwapani tuombeane uzima mwisho niwakumbushe wananchi ile hamasa yetu ya kujitokeza kwa wingi uwanjani imeishia wapi???? Jamani tusiwe wapenzi wa matokeo tukumbuke mpira una matokeo 3 : Kushinda ; Kutoka sare na Kufungwa. Niwakumbushe timu inaundwa na mfano najua ninyi ni wafuatiliaji wazuri wa soka angalia timu kama Liverpool kwa miaka kadhaa imekuwa washiriki lakini wanachama na wapenzi hawakukata tamaa walikuwa wakiisapoti timu yao leo tunaona wanachovuna, hivyo basi ” YANGA NEVER WALK ALONE ” Mwisho tujipongeze wananchi kwa kubadilika na kukomaa kisoka tushinde au tushindwe hatuna mambo ya kizamani ya kupigana bakora na badala yake tunajipanga tunajiuliza na kuusapoti uongozi kongole wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *