October 28, 2020

ALICHOSEMA MWAMBUSI KUELEKEA MECHI YA LIGI KUU DHIDI COASTAL UNION

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga juzi usiku iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Coastal Union kesho katika Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na chanzo chetu hapo jaba , Mwambusi alisema wachezaji wao ni wazuri na wanauwezo mkubwa, lakini wanahitaji kupata wachezaji ambao wanaweza kupambana kulingana na mpinzani wao wanayetarajia kukutana naye katika ligi hiyo.

Alisema mbali na kupata mwanga huo, lakini wanatengeneza ushindani mkubwa wa wachezaji wao kuhakikisha wanapata namba katika kikosi cha kwanza na kusaidia kupata matokeo chanya kwa kila mechi.

“Mechi hizi zinawasaidia kujiandaa na mchezo unaofuata wa ligi, lakini kutupa mwanga benchi la ufundi, kuona mchezaji gani atatusaidia katika mechi ipi, kuna jambo ambalo tunaliona ndani ya kikosi tunachokijenga ikiwamo kujenga ushindani zaidi kwa wachezaji wetu,” alisema Mwambusi.

Kuhusu mechi dhidi ya Coastal Union, Mwambusi alisema wanaimarisha kikosi chao kuhakikisha wanaendeleza moto wao wa kupata matokeo mazuri kwa kuvuna pointi tatu katika mechi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *