October 31, 2020

CARLINHOS ATENGA MUDA MAALUM, KUPIGA MISHUTI MAKALI

Msomaji wa Yanganews Blog:Si unaona zile kona bao za Carlinhos kwenye mechi za Yanga? Kama unafikiri jamaa huwa anazibahatisha ujue mapema utachekwa. Kiungo huyo kutoka Angola kumbe uchawi wake ambao umekuwa ukipagawisha mashabiki wa Jangwani na kuwapa presha mabeki wa timu pinzani huwa anaufanyia kazi kwa kutenga muda kila siku mazoezini ili kuzidi kuwa mtamu.

Msomaji wa Yanganews Blog:Juzi chanzo chetu lilimshuhudia kiungo huyo raia wa Angola akifanya mazoezi hayo katika uwanja wa ndani wa kambi ya AVIC iliyopo Kigamboni – nje kidogo ya mji, mara baada ya wenzao kuondoka walipomaliza mazoezi ya pamoja yaliyosimamiwa na Said Maulid ‘SMG’.

Kiungo huyo alikuwa akipiga mipira hiyo ambapo alionekana kutumia dakika zisizopungua 15-20 kupiga mipira hiyo, huku Kisinda akimuangalia na kumuelekeza alipoona anakosea.

Katika mipira 10, Carlinhos alilenga lango na kufunga mipira sita, huku minne ikipaa juu kidogo ya lango. Tangu atue Yanga, Carlinhos amekuwa akiwakuna mashabiki kwa umahiri wa kupiga kona zenye macho ambazo zimekuwa zikitia misukosuko lango la wapinzani.

Wakati Carlinhos akifanya yake, Kisinda alijaribu mipira kama hiyo, lakini zaidi alijielekeza kujaribu kukimbia kwa kasi na mpira kisha kupiga krosi katikati ya eneo la goli. Baada ya mazoezi hayo wawili hao walionekana kujadiliana mambo mbalimbali, kisha kuondoka kurejea kambini na kuonyesha kwamba kumbe wanachofanya katika mechi huwa wanavifanyia mazoezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *