October 28, 2020

TONOMBE AENDELEZA UBABE, YANGA IKIITUNGUA KMKM

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe ameendelea kufumania nyavu katika nafasi anazozipata na leo Septemba 30 amefanikiwa kuipa ushindi timu yake wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM kwenye mechi ya kirafiki.

Mchezo huo umepigwa leo uliaoanza saa 1 usiku katika Uwanja wa Azam Complex ambapo Yanga ilichezesha vikosi viwili na mabao yote yalipatikana kipindi cha kwanza.

Bao la kwanza Mukoko alimalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na mkali wa mipira hiyo Carlos Carlinhos dakika ya 10 na la pili dakika ya 30 beki wa KMKM alikosea kutuliza mpira, Mukoko alijitengea kisha kupiga shuti lililoenda langoni moja kwa moja.

Kiungo huyo ambaye alifunga pia kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar staili yake ya ushangiliaji kwa kuwakalisha wenzake chini na kuwa kama mwalimu imemfanya wampe jina la utani Ticha’ ikiwa na maana mwalimu.

Yanga ilicheza kwa mpira wa pasi na kushambulia kutoka pembeni mipira mingi haikuwa na faida kutokana na umakini mdogo wa washambuliaji wao kipindi cha kwanza akiwa Carlinhos na kipindi cha pili Michael Sarpong.

Kikosi cha kwanza Yanga kilichoanza kipa Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Adeyun Salehe, Makapu, Mwamnyeto, Makame, Deus Kaseke, Mukoko Tonombe, Yacouba Sogne, Carlinho, Tuisila Kisinda.

Nje ya uwanja mashabiki wa Yanga waliendeleza kuimba nyimbo za Amani wakibeba bango lililosomeka ‘Hatusapoti ngumi’ ikiwa ni ujumbe mzuri kwa tukio la mashabiki wa Simba kupigwa na kuzongwa lilitokea Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati wa mechi ya Yanga dhidi ya Mtibwa.

6 thoughts on “TONOMBE AENDELEZA UBABE, YANGA IKIITUNGUA KMKM

  1. ila yanga tunashinda kwa mpra ovyo ovyo tunaocheza kwa wachezaji hawa tuliokuwa nao yanga hii nilitegemea ingekuwa na kapumbu zuri lakuvutia lakini imekuwa kinyume chake kunamda naona afadhali hata kabumbu lile la akina moringa kuliko yanga hii na hilii nitatizo uwezo wa huyu mwalimu mdogo sana kwa mtazamamo wangu

  2. navuta kumbukumbu mwanayanga mmoja anaitwa dcdoublekey aliona mbali tena kwenye jicho la3 alivyoongerea gam ya yanga na kagera wiki mbili zilizopita kuwa uwezo wa yanga kwa mpira uliochezwa kipindi cha kwaza afadhali yanga ile ya akina moringa watu walishindwa kumwelewa kumbe ni kweli na ndiyo uhalisia sasa tunaaza kumwelewa kwa nini alimaananisha vile kama sisi tunaona mpira haufulahishi nina imani pia gsm na uongozi hili mnaliona kseni chini na kocha muuonge nae mapema tunaumia sana na tunaipenda yanga yetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *