October 28, 2020

MWAKALEBELA AWEKEA MSISITIZO, TUSIWAPIGE MASHABIKI SIMBA

Msomaji wa Yanganews Blog:Uongozi wa Yanga umesema kuwa kwa sasa ni muhimu mashabiki wake wakaelewa kwamba mpira sio uadui bali ni mwendelezo wa upendo na mshikamano katika kila jambo ambalo wanalifanya hivyo ni muhimu kwao kuacha kabisa tabia hiyo.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa kwa sasa elimu inaendelea kutolewa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mpira ili kuweza kuondoa kabisa tatizo hilo.

“Mashabiki wa Yanga wanapaswa waelewe kwamba mpira sio uaduia ni furaha na mshikamano, kwa sasa elimu inazidi kuendelea kutolewa lengo ikiwa ni kupunguza na kuondoa kabisa hili tatizo.

“Kwa mashabiki wa Simba, Yanga sisi sio maadui bali tunafanya ule utani wa jadi, jukumu ni letu pia tuna kazi ya kufanya kama ilivyokuwa zamani ambapo utani ulikuwa ni kwenye mpira pekee ila upendo unadumu huku kwenye shida wakiwa pamoja ikiwa ni kwenye misiba hivyo muhimu kuendeleza utamaduni,” amesema.

4 thoughts on “MWAKALEBELA AWEKEA MSISITIZO, TUSIWAPIGE MASHABIKI SIMBA

  1. Upinzani wa Jadi upo tooa asili na haya hayakuwepo ila wapenzi wa simba wamezidi wakiongozwa na manara kwanza tff wamchukulie hatua manara kwa kauli zake za kuudhi na kukashifu. Wapenzi wa yanga sio vichaaa, haijawahi kutokea simba anacheza wapenzi wa yanga wakenda kukaa kwenye jukwaa la simba ña kutoa kauli za maudhi kwa wapenzi wa simba na simba yenyewe. KWA YANAYOTOKEA HIVI SASA TFF NA MANARA NDIO WAHUSIKA WAKUU

  2. Tumevumilia sasa tumechoka kejeli za manara ana tutukana sana kwa mgongo wa utani, nishukru uongozi kwa ujumbe wenu. lakini chanzo cha vurugu ni wanasimba wenyewe wanamaneno mazito ambayo kuvumilia ni kazi kama wewe ni shabiki/mwanachama wa yanga, Ombi langu ni kwa viongozi wa yanga simba Tff Elimu ienderee kutorewa kwa wapenzi wa mpira vinginevyo tutaenderea kuwanyosha hadi ligi iishe maana kwenye nembo yetu kuna bondia

  3. Hata kuwadunda na kuwachania nguo bado ni muendelezo wa utani tu, so ni utani tu. Simba wasihamaki! Waambie hao simba, ulikuwa ni utani tu na wauchukulie kuwa ni UTANI TU!

  4. nikweli makamu mwenye kiti lakini ukumbuke kua haya yote yanasababishwa na tff pia mara hebu kumbuka utani wa 2010 mpaka 2014 ulivyo kua utani wa jadi jadi kweli lakini hawa wabwatukaji akiwemo manara kutukana matusi kejeli hadhalani lakini tff hawana hatuwa wanazo zichukua dhidi yao je wafikili kwa hali hiyo kutakua na utani mzuli kama ulio kua wachezaji wa zamani akiwepo Ali mayay tembele ilikua soka la kuigwa pia utani ulikua utani kweli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *