October 28, 2020

KISINDA ATAJA UWANJA TATIZO KUSHINDWA KUONESHA MAKEKE JAMHURI

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Yanga, Tuisila Kisinda amesema hana shida katika kucheza kwenye viwanja vya ubora wa kawaida lakini ule wa Jamhuri ni kiboko.

Akizungmza mara baada ya mchezo huo Kisinda amesema uwanja huo hauna hadhi ya kuchezewa mechi za Ligi kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea.

Winga huyo Mkongomani amesema hali ya uwanja huo unamlazimu mchezaji kutumia muda mrefu kumiliki mpira na kumnyima uhuru wa kufanya anachotaka kukifanya.

“Mpira hautulii kila ukitaka kujipanga unakuta tayari wapinzani wamefika eneo hilo, ni uwanja mbovu sana uliniudhi, amesema Kisinda.

“Sina tatizo katika kucheza kwenye viwanja vya kawaida lakini huu wa Jamhuri ulikuwa mbovu zaidi na hauna hadhi kabisa ya kuchezewa Ligi kubwa kama hii.

Aidha Kisinda akizungumzia hatua ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuufungia amesema uamuzi huo ni sahihi na kwamba anaunga mkono na kuwataka wahusika kuutengeneza.

“Wamefanya uamuzi sahihi kabisa sio uwanja mzuri wanatakiwa kuutengeneza unazifanya timu kucheza nje ya malengo yao.

3 thoughts on “KISINDA ATAJA UWANJA TATIZO KUSHINDWA KUONESHA MAKEKE JAMHURI

  1. Kitendo walicho fanyiwa Simba sikiungwana lakini niswa kwakuwa walikwenda kuwakera Yanga na tambo zao zakijinga huku wakijua nikosaaa wanayanga unapokwenda tunapokaa karibu na wanasimba huwahatujui kuchonga midomo na huwa tumefunga midomo huwezi kwenda kwenye nyumba ya jirani ukamtukana na kumdhalilisha akakuwacha walichopata Simba ni malipo ya mdomo wao Wana muiga Manara na Manara anatukania Yanga mbali nawametumwa na Manara yaani ipohivi Simba hawatakiwijukwaa la yangaa au Yanga jukwaa la simba kila mtu kivyakebasii sisi Yanga Simba ni nuksi na balaa

  2. ujue cku zote kama mtu huna akiri ya kujiongeza lazima uteseke mpira n mhemko mkubwa na bnadam tunatofautian mihemko so tumia akiri kabla haijakutumia ilipaswa shabik wa cmba walitambue hili yasingetokea hayo yote by zakaria aka Z Mac

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *