October 28, 2020

ZLATKO ALIANZISHA KUSUKA SAFU YA USHAMBULIAJI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic amesema kwa sasa anachokiangalia ni kupata mabao kwa wingi kutokana na kutoridhishwa na ushindi wa goli moja ukizingatia timu hiyo ina wachezaji wengi wazuri wenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Zlatko alisema pamoja na kikosi hicho kuendelea kupata muunganiko taratibu, matarajio yake ni kuona mabao mengi yanaendelea kupatikana kadri wanavyoendelea kucheza mechi za ligi hiyo.

“Kikosi kipo vizuri, lakini kwa sasa ninachokiangalia ni kuhakikisha nawapa wachezaji mazoezi ambayo yatawafanya waweze kuwa na uwezo wa kufunga magoli mengi zaidi pindi tunapokuwa uwanjani,” alisema Zlatco

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *