August 13, 2020
Breaking News

NUGAZ AWATOA HOFU WANAYANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amewataka wapenzi na wanachama wa timu hiyo kuwa wavumilivu kwa kila jambo wanalolisikia kuhusu timu yao.

Nugaz aliwasili makao makuu ya timu hiyo na kupokelewa na wafuasi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi kujua hatma ya yale wanayoyasikia kuhusu timu yao huku kubwa wakingoja kusikia hatma ya Benard Morrison ambaye suala lake lipo TFF.

“Hawawezi kushindana na sisi, timu yetu inaongozwa na viongozi vijana na hawaogopi mtu, niwaombe muwe watulivu kwani kila kitu kinakwenda vizuri na limefikia asilimia 98,” alisema Nugazi.

Pamoja na furaha ya kusikia suala la Morisson linakwenda vizuri kwa upande wao, mashabiki wengi walisikikika wakisema hawamtaki tena maana atakuja kuwasumbua mbele ya safari.

Mashabiki hao walianza kumiminika viunga vya makao makuu ya timu hiyo, wakiwa na hamu pia ya kutaka kujua usajili mpya utakaotangazwa siku ya leo huku asilimia kubwa wakiwa wanafuatilia mitandao ya kijamii ili kujua kinachoendelea, baada ya tetesi zinazoelezwa, mchezaji wa Simba, Clatous Chama na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems kuwa nao wapo njiani kutua Jangwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *