August 13, 2020
Breaking News

USAJILI YANGA KUKAMILISHWA HIVI KARIBUNI

Msomaji wa Yanganews Blog:Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa kwenye suala la usajili katika klabu hiyo hakuna shida kabisa, kwani mambo yameshaanza na yanakaribia kumalizika baada ya wiki moja au mbili hivi.

“Mipango iko vizuri kwa wachezaji wa kimataifa ambao ndiyo kwa sasa tunaangalia, lakini kwa hawa wa ndani hakuna shida kabisa, tumeshakamilisha usajili wa wachezaji wa Kitanzania kwa asilimia 90, tena wale tuliokuwa tunawahitaji, alisema Bumbuli.

Alisema kuwa wachezaji wote hao wamesajiliwa baada ya kupendekezwa na benchi la ufundi.

“Tuna muda wa wiki moja au mbili hivi wa kukamilisha usajili wachezaji wa ndani, wale ambao benchi la ufundi waliopendekeza au kutafuta mbadala wao kama itashindikana kuwapata wote,” alisema.

Hata hivyo, wakati Bumbuli akisema hayo, tayari klabu hiyo imeshamfukuza Kocha wao Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji baada ya kunukuliwa akiongea maneno yanayoashiria ubaguzi.