July 8, 2020
Breaking News

LEO PATACHIMBIKA DIMBA LA TAIFA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema wanahitaji kulipa kisasi katika mechi ya hatua ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar inayotarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Yanga itashuka katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 3-0, walichopata mara ya mwisho wakipokutana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na chanzo chetu jijini jana, Eymael alisema anaandaa kikosi cha ushindi na anaamini wako tayari kulipa kisasa kwa kuwaondoa Kagera Sugar katika mashindano hayo.

Eymael alisema hataki kupoteza mechi hiyo na hawako tayari kumbukumbu ya kichapo kutoka kwa timu hiyo ijirudie katika mchezo huo ambao utawasaidia kuendelea na safari ya kusaka nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Alisema anawaheshimu Kagera Sugar ni timu yenye wachezaji wazuri na wataingia uwanjani kupambana kutafuta matokeo chanya katika mchezo wao huo  utakaokuwa wa ushindani kwa pande zote.

“Hii ni mechi ngumu sana kwa pande zote mbili, binafsi tunahitaji kulipa kisasi pia kuhitaji kucheza nusu fainali ili tuje kucheza fainali ya FA michuano ya FA ndio itatuongoza kushiriki michuano ya kimataifa, tuko makini,” alisema Eymael.

Mechi nyingine ya robo fainali ya michuano hiyo itakayochezwa leo itakuwa ni kati ya Sahare Stars dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

8 thoughts on “LEO PATACHIMBIKA DIMBA LA TAIFA

  1. Very good article! We are linking to this particularly great content on our site. Keep up the great writing.

  2. Kila raheri benchi la ufundi na wachezaji,hima tutavuka ;…keep it up…

  3. Nawaomba sana viongozi wajuu wakubaliane na mabadiliko. Dunia ya sasa ni yakisasa.YANGA Oyeeeee.Daima YANGA nyuma MWIKO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *