July 8, 2020
Breaking News

KASEKE AZUNGUMZIA ALIVYOITUNDIKA NDANDA

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Yanga, Deuse Kaseke ameeleza kwa kina jinsi alivyofanikiwa kuwasoma mabeki wa Ndanda FC na kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara mwishoni mwa wiki.

Amesema pamoja na kwamba mabeki wale ni warefu kuliko yeye, alijitahidi sana kusoma mwenendo wa mpira kutoka kwa wachezaji wenzake kisha kukaa kwenye eneo ambalo alijua anaweza kuucheza mpira kabla ya kuwafikia walinzi wa Ndanda FC.

“Nilikuwa nawasoma mabeki walivyo, bao la kwanza niliona wote wamesimama, na kwa kasi ya nchimbi nilijua krosi itafika hivyo nilijitosa katikati yao na kweli nikauwahi mpira na kufunga bao,” anasema.

3 thoughts on “KASEKE AZUNGUMZIA ALIVYOITUNDIKA NDANDA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *