July 8, 2020
Breaking News

ALICHOSEMA JUMA ABDUL KUELEKEA MECHI KOMBE LA FA DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Akizungumza na chanzo chetu hapo jana, jijini Dar es Salaam, Abdul alisema lengo ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili waweze kufikia malengo ya kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

Alisema kuwa pia mchezo huo ni maalum kwao kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 na wapinzani wao hao katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa.

“Wachezaji wote tuko vizuri na morali ya hali ya juu, hivyo tunajipanga kisawasawa kuhakikisha tunarudisha kisasi kwa Kagera ambao walitufunga 3-0 na sisi tunataka kuutumia mchezo huu kulipa kisasi,” alisema Abdul.

Deus Kaseke aliyeifungia Yanga mabao mawili walipovaana na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara juzi Jumamosi, alisema kuwa wapo fiti kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Kagera Sugar kesho.

“Tupo vizuri, tumejipanga kupata ushindi tutakapocheza na Kagera, mashabiki waje kwa wingi uwanjani,” alisema Kaseke akiungwa mkono na nyota wenzake wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa ambaye naye alitupia dhidi ya Ndanda katika ushindi wa mabao 3-2.

6 thoughts on “ALICHOSEMA JUMA ABDUL KUELEKEA MECHI KOMBE LA FA DHIDI KAGERA SUGAR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *