July 8, 2020
Breaking News

BALAMA AWASHUKURU WACHEZAJI, MASHABIKI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Yanga, Mapinduzi Balama amesema amejisikia faraja kubwa kuona wachezaji wenzake wakimtakia heri mbele ya mashabiki wa timu Uwanjani.

“Nimefarijika sana, huu ni upendo wa hali ya juu, nawashukuru sana wenzangu kwa namna walivyoguswa na tatizo langu na kwa ushirikiano mkubwa wanaonipatia,” amesema Balama.

Amesema anathamini sana upendo ulioonyeshwa juu yake, lakini pia anawashukuru sana mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kwa namna wanavyompa pole na kumtia moyo katika wakati huu.

“Kwa namna ya kipekee pia anawashukuru Wanayanga wote kwa jinsi wanavyomfariji kwa ujumbe wao kupitia vyanzo mbalimbali, wananipa moyo nami naamini nitarejea kuipambania timu yangu,” amesema.

Balama aliumia mazoezini kwa kuteguka kifundo cha mguu na kuvunjika mfupa mdogo wa pembeni ya mguu.

15 thoughts on “BALAMA AWASHUKURU WACHEZAJI, MASHABIKI YANGA

  1. Dawa ya mchezaji msumbufu ni atafutwe mmbadara wake yeye achome mahindi au aote moto tu

  2. polesana mungu atakupa wepesi ningeuwomba uongozi ufanye kila linalo wezekana kumpatia matibabu makubwa na huduma muhimu msimterekeze nikipindi chakuthamini mchango wake

  3. polesana ndugu yangu Mungu akupe nafuu haraka wewe ni miongoni mwa wapambanaji ninao wakubari Sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *